![]() |
![]() |
Courses« Home TIRDO now conducts several courses in different aspects with the highly qualified instructors from different departments of the organization. The courses taught so far are as follows: Welding and Fabrication Mafunzo ya uchomeaji wa vyuma vya aina zifuatazo; vyuma vya kawaida (Ferrous materials), stainless steel na aluminium pamoja na mafunzo ya uchomeaji wa kitaalamu. Mushroom Farming Mafunzo juu ya kilimo cha uyoga (Mushroom Farming) kutoka kwa wataalamu waliobobea katika kilimo hicho. Welding and Fabrication Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) linaendesha mafunzo ya uchomeaji wa vyuma vya aina zifuatazo; vyuma vya kawaida (Ferrous materials), stainless steel na aluminium pamoja na mafunzo ya uchomeaji wa kitaalamu. Kila kozi itakuwa na mafunzo ya nadharia na vitendo katika kuwaendeleza wachomeleaji wa kawaida. Pindi mafunzo yatakapoisha wachomeaji watakuwa na uwezo wa kutengeneza bidhaa bora pamoja na kuweza kukagua kiufundi. Mafundi wa TIRDO wakionesha jinsi ya kufanya uchomeleaji stadi Malengo Ya Kozi: Programu ya mafunzo ya kuongeza ufundi yatawaongoza wachomeaji katika maeneo yafuatayo; Elimu ya msingi ya ufundi. Njia mbalimbali za uchomeaji. Kuanzisha na Kuendesha Mfumo Bora wa Uchomeleaji: Kugundua tatizo na kulitatua Usalama kazini Kupambanua aina za uchomeleaji Kutathmini uchomeleaji Sifa za Wawezeshaji/Wakufunzi: Wakufunzi wote wamefuzu cheti cha ASME code selection IX na wana uzoefu mkubwa katika uchomeleaji. Matarajio: Hii kozi inatarajiwa kuwa itawasaidia washiriki kuzalisha bidhaa na huduma bora kutokana na ujuzi bora watakaopata. Washiriki Watanufaika na Yafuatayo: Kuelewa kanuni za uchomeleaji. Kuanzisha na kuendesha mfumo bora wa uchomeleaji Kudhibiti matatizo mbalimbali ya uchomeleaji. Anayetakiwa Kushiriki: Mafundi wachomeleaji. Wachomeleaji wasio na uzoefu Wasimamizi Wakaguzi wa ubora Tunuku: Baada ya kumaliza kozi, mhitimu atatunukiwa cheti. Gharama ya Kozi: Kila mshiriki atatakiwa kulipa ada kutegemea na kozi. Mushroom Farming Tanzania Industrial Research and Development Organization (TIRDO) tunatoa mafunzo juu ya kilimo cha uyonga (Mushroom Farming) kutoka kwa wataalamu waliobobea katika kilimo hicho. Katika kozi hii tunafundisha mambo yafuatayo kwa wale ambao watahitaji kufahamu kuhusu Uyoga:- Kilimo cha uyoga kuanzia kutayarisha vimeng'enywa hadi kupanda. Utunzaji wa shamba,uvunaji,ufungashaji na uhifadhi. Mapishi ya uyoga kwa nadharia na vitendo Course Duration: 1 week (08:00-1400hrs daily Monday-Friday) Course Fee: 20,000 Tsh Maulizo yote yaelekezwe kwa: Mkurugenzi Mkuu, TIRDO Mtaa wa Kimweri, Msasani P.O.Box 23235 Dar es Salaam
Simu: 255 22 2666034/2668822 Fax: 255 22 2666034
|
![]() |
![]() |
| Home | About Us | ICT Unit | Vacancies | Contact Us | Sitemap |
| © Copyright TIRDO. All right reserved. |